Ureno vs USA: Fahamu matokeo na wafungaji hapa
Baada ya kupoteza mechi ya awali kwa kipigo cha goli 4-0 kutoka kwa Ujerumani, usiku wa jana timu ya Ureno ilicheza mechi yake ya pili kwenye michuano ya kombe la dunia.
Ureno wakiongozwa na nahodha wake Cristiano Ronaldo walipata sare ya bao 2-2 dhidi ya USA.
timu ya Ureno ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika za mwanzo za mchezo kupitia kwa mchezaji wake Luis Nani, na baadae Marekani wakasawazisha kupitia kwa Jermaine Jones, na zikiwa zimebaki dakika tisa tu mpira kumalizika, mshambuliaji wa USA Clint Dempsey akafunga goli la pili.
Huku mashabiki wa Ureno wakijua timu yao imeshapoteza mechi, Cristiano Ronaldo akatengeneza krosi kwenda kwa Varela aliyefunga goli la kusawazisha kwenye dakika ya mwisho kabisa ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 2 - 2

Post a Comment