Arsene Wenger afunguka kuhusu Kylian Mbape
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amefunguka na kuzungumzia tetesi zilizokuwa zikisambaa kuhusu timu yake kutaka kumsajili mshambuliaji wa monaco - Kylian Mbape.
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Arsenal na Western Sydney wanderers hapo jana, Wenger alizungumza na kusema kuwa klubu yake haija wasilisha bid yoyote kumtaka mchezaji huyo wa monaco.
Arsene Wenger ana amini kuwa Kylian Mbape ataendelea kuichezea Monaco.
Mbape hivi sasa thamani yake ni zaidi ya pound millioni 100.
Vile vile Arsene Wenger amezungumzia kuhusu tetesi za kuuzwa kwa Oxlade-Chamberlain ambae inasemekana kuwa Chelsea wana mtaka.
Arsene Wenger amesema kuwa mchezaji huyo hata ondoka Arsenal kwa sasa kwani bado anahitajika.
Mpaka sasa Arsernal imesha fanya usajili wa mshambuliaji Alexandre Lacazette amabe amesajiliwa kwa poundi milioni 52
Post a Comment