Wasanii wa serengeti fiesta Tanga wakimsabahi mzee njenje
Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Mzee Njenje (kushoto), akiongea na wasanii wa muziki wa kizazi kipya walipomtembelea nyumbani kwake mjini Tanga , msanii huyo kwa sasa anasumbuliwa na matatizo ya kiafya. Wasanii hao wapo katika msafara wa tamasha ya Serengeti fiesta ambapo kwa mjini hapo linafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya , Jux akimsalimia msanii mkongwe wa dansi, Mzee Njenje wakati wasanii hao walipomtembelea nyumbani kwake mjini tanga , kabla ya onyesho la Serengeti fiesta kufanyika mjini humo leo jioni
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba (kushoto) na Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney wakiteta na Masanii mkongwe wa muziki wa dansi, Mzee Njenje alipotembelewa na timu ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ili kumpa mkono wa pole.
mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Mzee Njenje (wa tatu kulia) waliokaa, akipozi kwa picha na baadhi ya wasanii Serengeti fiesta pamoja na baadhi ya watu wengine wenye mapenzi mema walimpomtembelea nyumbani kwake mjini Tanga.
Post a Comment